“Jiko langu linajali afya yako”

Shuhuda

Nimepokea shuhuda za Maelfu ya Watanzania tangu nianze kufundisha Mbinu za Mapishi yenye kuzingatia lishe bora kwa kutumia nyenzo maarufu kama SAYANSI YA MAPISHI. Wewe pia unaweza kuwa mwanafunzi wangu ukanufaika na Jiko langu.

Kitambi

Tatizo ambalo linatesa jamii na kumhatarisha kupata magonjwa karibia yote ya lishe. Ingawaje ni asilimia ndogo sana ya Watanzania wanajua kwa kina juu ya sayansi ya kitambi. Ili kuweza kukabiliana na ongezeko la kasi ya watanzania wenye uzito uliokithiri na kitambi niliamua kuanza kufundisha jamii kwa ngazi ya chini ili ajue kwanza Kitambi kinatokeaje ili tuweze kuweza kukabiliana na tatizo hilo tukiwa na uelewa wa kina. Kitambi sio ulafi wala uvivu wa mazoezi. Katika madarasa yangu utajifunza nadharia zote zinazo sababisha kitambi. Ulafi na uzembe wa mazoezi ni dalili za kitambi kwa mujibu wa nadharia zote za sayansi ya mapishi. Kwa sababu Mtanzania hajui chanzo halisi cha kitambi usitarajie ataweza kujikinga asipate kitambi na magonjwa yote ya lishe. Kitambi ni mpasuko wa afya endapo usipoziba utajenga ukuta. Wengi hupuuza kitambi na kuona ni jambo la kawaida kumiliki Kitambi kulingana na mitizamo hasi kwa kila mtu.

Ugumba

Asilimia kubwa ya wanawake na wanaume wanahatarisha miili yao katika matibabu yenye kugharimu pesa nyingi na afya zao kiujumla kwa lengo la kupata mtoto huku wakiwa hawana hata nuru juu ya mchango wa lishe bora katika kukuhakikishia unapata mtoto wako. Vyakula vya sukari na wanga sayansi inatuonesha kwamba ndivyo vinaongoza katika kuvuruga vichocheo vya mwanamke na mwanaume na kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kupevusha mayai na mwanaume asiwe na uwezo wa kuweka mbegu kwenye kizazi na kutengeneza mbegu zakutosha. Kupitia sayansi ya mapishi, nimepokea shuhuda nyingi wanawake wengi wenye PCOS wamebeba ujauzito na wanaume wengi nguvu za kiume zimerejea ndani ya miezi sita wakitekeleza Kanuni hizi jikoni.

Kisukari

Ugonjwa ambao tuna mamlaka ya kuikinga jamii na tuna mamlaka ya kuudhibiti usilete uharibifu wowote kwa mgonjwa anayeishi na kisukari. Jiko letu nimerudisha tabasamu la maelfu ya watanzania ambao walikuwa hawana matumaini kabisa ipo siku wataondokana na mateso ya kisukari. Hii inadhihirisha kwamba kwa kutumia chakula bora hakuna ugonjwa wa lishe ambao ni “sugu na usiodhibitika” Wewe hautakuwa mtu wa kwanza kunishuhudia juu ya kisukari. Hakikisha unafuata kanuni zote za mapishi kulingana na mafunzo yangu hatua kwa hatua kwa miezi 3 mpaka 6 utakuwa umepiga hatua kubwa sana

Timu yetu

Tupo kwaajili yako

Dr Boaz Mkumbo MD

Mwanzilishi wa HEALTHY EATING ACADEMY

Ni Daktari wa magonjwa wa binadamu (Doctor of medicine), mwandishi wa vitabu na mwelimishaji maarufu wa Afya jamii amejikita katika magonjwa ya lishe. Kupitia program yake maarufu kama HeA na akitumia nyenzo ya matibabu maarufu kama SAYANSI YA MAPISHI amegusa maisha ya maelfu ya Watanzania na nchi za karibu kama Uganda,Burundi,congo na kenya. Amekuwa akisema “Sikutarajia kuona jamii ina kiu kikubwa kiasi hiki juu ya elimu ya magonjwa ya lishe, nimeshindwa hadi kutimiza haja yao hata kufikia nusu ya uhitaji wa elimu hii”. Hii inatokana na sababu mbalimbali kama nguvu kazi kidogo, kukosa watu wenye wito wa kujitolea kufundisha na upungufu wa fungu la pesa kuwafikia hata wasioweza kulipia elimu hii hata gharama za usafiri na maradhi kwa wakufunzi. Ameamua kutumia njia mbalimbali kugusa maisha ya watu wenye magonjwa ya lishe kwa kuwekeza muda wake wote kutoa mafunzo bure kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook,Youtube na Instagram. Mbali na hivyo ameandika vitabu mbalimbali ambavyo vinatumika kama mwongozo katika Ofisi yake kwa yeyote anayetaka kujitibia magonjwa ya lishe kwa kutumia kanunu na misingi ya HeA jikoni.

LUZAMA F KAZULA

Meneja wa Mradi Healthy Eating Academy

MARTHA PROSPER

Customer Care

FIKIRA NYARUSI

Personal Secretary

DORA

Sales Represantative

RICHARD MAGULUKO

Graphics designer

ROBERT TILUSASILA

Sales Represantative

Close Menu